KIDS GENERATION
#Watoto na vipaji
Sheila Sheldon ana umri wa miaka 9 pekee lakini uchoraji wake ni wa kiwango cha juu ikilinganishwa na watoto wa rika lake.
Yeye huchora picha ili kujifurahisha lakini cha kushangaza ni kwamba licha ya kuanza uchoraji akiwa na umri wa miaka sita hajapata mafunzo yoyote ya uchoraji.
Na tayari ameanza kugonga vichwa vya habari baada ya kuchora picha ya Rais Uhuru Kenyatta na kuvutia mwaliko katika ikulu ya rais huyo wa Kenya.
Vile vile amewahi kuchora picha za Gavana wa Mombasa Hassan Joho, Gavana wa Kwale Salim Mvurya na mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir.
Kipaji cha uchoraji wake kwanza kiligunduliwa katika shule ya kimataifa ya Diani International School.

