WATOTO NA VIPAJI.
Msichana kutoka Githurai nchini Kenya, Gracious Amani ‘Amani G’ aliyemkuna Staa wa muziki kutoka Marekani, Alicia Keys kwa uwezo wake wa kuimba wimbo wa ‘ Girl On Fire’,Julai 17 2018 aliingia Location na Director wa video za muziki wa nchini humo, Young Wallace.
Msichana huyo anayesoma Darasa la Nane katika shule ya msingi Githurai nchini humo, tayari alishatangazwa kuwa atatumia jina la sanaa kama ‘Amani G’ na kwa sasa anafanya kazi zake za muziki chini ya lebo ya muziki ya Pine Greek Records iliyoko Nairobi nchini humo inayomilikiwa na Peter Nduati.
#NEW_GENERATION_WITH_CHANGES

