Contact Form 0742667518
July 29, 2018
Kombe la New kings limeendelea leo Julai 29,2018 katika uwanja wa Shule ya msingi Tungi iliyopo kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro ikiwa ni nusu fainali ya kwanza iliyoziusisha Timu za Care Youth Foundation Football Team(CYF FT) na Young Star,mchuano uliomalizika dakika 90 kwa Timu ya Young Star kuibuka na ushindi wa Mabao 4-1 hivyo kuifanya Timu ya Young Star kumsubiria msindi wa mchezo wa kesho kati ya New Kings(Wadhamini wa kombe) na Bodaboda Fc mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Shule ya msingi Tungi saa 10:00 jioni.
Mshindi wa kombe hilo atapewa zawadi ya Mipira miwili.
Ikumbukwe kuwa Timu ya Care Youth Foundation Football Team( CYF FT) yenye wachezaji wenye chini ya Umri wa miaka 25 ipo chini ya Asasi ya CARE YOUTH FOUNDATION(CYF) inayojiusisha na masuala ya kijamii kama kama vile kutoa elimu ya Afya, mazingira, ujasiriamali,utawala bora pamoja na kufanya tafiti mbalimbali. Makao makuu ya Asasi yapo Mkoani Morogoro.
Subscribe to:
Posts (Atom)


