Contact Form 0742667518

Name

Email *

Message *

September 26, 2018

Msomaji na mfatiliaji wa habari na taarifa zinazowahusu Watoto kupitia katika ukurasa  wa #Facebook. Blog ya #KIDS_GENERATION na   #Instagram  leo tuangazie sheria ya haki za Mtoto ya mwaka 2009 kipengere cha **kazi za Mtoto**:

"Watoto wana ruhusa ya kufanya kazi baada ya kutimiza 
umri wa miaka 14. Kazi haipaswi kumzuia mtoto kuhudhuria 
masomo au kupata muda wa kujisomea na kupumzika. Watoto 
wasiajiriwe kufanya kazi nyakati za usiku.
Yeyote anayewafanyisha kazi watoto kupita kiasi, au asiyewalipa 
ujira unaostahili, basi anavunja sheria hii.
Ni makosa kuajiri mtoto kama kazi anayopaswa kufanya ni ya 
hatari. Watoto hawaruhusiwi kufanya kazi za baharini, kwenye 
machimbo au eneo la kupasua mawe na kokoto, wala kubeba 
mizigo mizito au kufanya kazi zinazotumia kemikali au mitambo. 
Watoto hawaruhusiwi kufanya kazi za hotelini wala vilabu vya 
pombe."




Pamoja na kwamba Sheria zimefafanua kipengere hicho kwa kina lakini katika jamii zetu bado kuna Watu bado wanawatumia Watoto kufanya kazi za uzarishaji jambo linalipelekea wakose haki zao za msingi hasa ELIMU .
KIDS GENERATION inapenda kuwakumbusha Wazazi,Walezi, Mashirika, Taasisi za Kiserikali na watu BINAFSI kulivalia juga swala hili na kuchukua hatua kali sana kwa yeyote atakayekwenda kinyume  ili kuleta ustawi katika jamii husika na Taifa kwa ujumla.

Tunza,
Linda,
Heshimu haki za Mtoto.

   #New_generation_with_change