Msomaji na mfatiliaji wa habari na taarifa zinazowahusu Watoto kupitia katika ukurasa wa #Facebook. Blog ya #KIDS_GENERATION na #Instagram leo tuangazie sheria ya haki za Mtoto ya mwaka 2009 kipengere cha **kazi za Mtoto**:
"Watoto wana ruhusa ya kufanya kazi baada ya kutimiza
umri wa miaka 14. Kazi haipaswi kumzuia mtoto kuhudhuria
masomo au kupata muda wa kujisomea na kupumzika. Watoto
wasiajiriwe kufanya kazi nyakati za usiku.
Yeyote anayewafanyisha kazi watoto kupita kiasi, au asiyewalipa
ujira unaostahili, basi anavunja sheria hii.
Ni makosa kuajiri mtoto kama kazi anayopaswa kufanya ni ya
hatari. Watoto hawaruhusiwi kufanya kazi za baharini, kwenye
machimbo au eneo la kupasua mawe na kokoto, wala kubeba
mizigo mizito au kufanya kazi zinazotumia kemikali au mitambo.
Watoto hawaruhusiwi kufanya kazi za hotelini wala vilabu vya
Pamoja na kwamba Sheria zimefafanua kipengere hicho kwa kina lakini katika jamii zetu bado kuna Watu bado wanawatumia Watoto kufanya kazi za uzarishaji jambo linalipelekea wakose haki zao za msingi hasa ELIMU .
KIDS GENERATION inapenda kuwakumbusha Wazazi,Walezi, Mashirika, Taasisi za Kiserikali na watu BINAFSI kulivalia juga swala hili na kuchukua hatua kali sana kwa yeyote atakayekwenda kinyume ili kuleta ustawi katika jamii husika na Taifa kwa ujumla.
Tunza,
Linda,
Heshimu haki za Mtoto.
#New_generation_with_change



No comments:
Post a Comment