Contact Form 0742667518

Name

Email *

Message *

August 01, 2018

LINDA,TUNZA ,HESHIMU HAKI ZA WATOTO.


Taarifa ya Shirika la kuhudumia Watoto duniani (UNICEF) ya 06 Machi 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto, Unicef limesema kuwa kuna mafanikio makubwa ya kupungua kwa ndoa za utotoni duniani.

Shirika hilo la Unicef limekadiria kuwa ndoa za utotoni zipatazo milioni 25 zimeweza kuzuiliwa katika muongo iliyopita.

Kwa sasa ni msichana mmoja kati ya watano anaolewa chini ya miaka 18 tofauti na miongo iliyopita ambapo ilikuwa msichana mmoja anaolewa kati ya wanne.

Shirika hilo la watoto limesema Kusini mwa nchi za bara la Asia wamejitahidi zaidi katika kupunguza ndoa za utotoni.

Anju Malhotra, mshauri wa masuala ya jinsia kutoka Unicef anasema haya ni mabadiliko mazuri katika maisha ya wasichana wote duniani hivyo upunguaji wa vitendo hivyo hata kwa kiwango kidogo ni habari njema ingawa bado kuna safari ndefu ya kutokomeza ndoa hizo za utotoni.

Hapa kuna ufafanuzi wa hali harisi ya Afrika ya Mashariki 

Kwa mujibu wa takwimu za Unicef za kati ya mwaka 2010 na 2017, Tanzania ni ya tatu kwa kuwa na viwango vya juu vya ndoa za utotoni baada ya Sudan Kusini na Uganda.

Sudan Kusini kiwango cha watoto wa chini ya miaka 18 wanaoozwa ni asilimia 52 na nchini Uganda ni asilimia 40. Tanzania ni asilimia 31.

Nchini Kenya, ni watoto asilimia 23 wanaoozwa kabla ya kutimiza miaka 18.